Kijiji/kituo Kwa maisha yajayo

Kijiji/kituo kitaitwa ‘Angaza Children’s Village’. ‘Angaza’ ni neno la Kiswahili linalomaanisha “kuangaza’ kitakuwa makazi rafiki kwa watoto hadi 60 ambayo tunataka kujenga. Hiki ndicho ambacho ZAC inataka kutoa kwa watoto itakaowalea. Tutajenga kwenye eneo lenye ukubwa wa kilometa za mraba 90,000 ambalo tumepewa bure na Mohammed Enterprises Tanzania Limited ( MeTL)

Katika eneo letu la ujenzi, tunataka kujenga jumla ya nyumba 5 za kifamilia za kuishi, kila nyumba watoto 12 wataishi na kelelewa. Kila nyumba itajengwa kwa matofali ya saruji na itakuwa na paa lililoezekwa kwa vigae. Na kila nyumba itakuwa na vyumba vitatu vya kulala kwa ajili ya watoto hadi 12. Kila nyumba itakuwa na mlezi wake atakayeitwa ( Mama wa nyumba) ambaye atakuwa na chumba chake pekee kwa ajili yake.

Moyo wa kijiji/kituo utakuwa ni chumba kikubwa cha mkutano, ambapo watoto wataweza kukutana kirafiki katika chumba cha chakula kwa ajili ya kupata vyakula vyao. Chumba hicho cha mikutaano kitakuwa pia na jiko na stoo ambacho kitaongezwa kulingana na mahitaji ili kiweze kukidhi mahitaji ya watoto. Vifaa vya usafi kama bafu, sehemu za kuogea za chini na vyoo vitakuwepo pia katika jengo hili kubwa la mikutano.

Außenansicht des zweiteiligen Gemeinschaftshauses.

Mwonekano wa nje wa Jengo la Mikutano (caption]

Kijiji kwa maisha ya baadae

Imepangwa kwamba, majengo makuu katika kijiji/kituo cha watoto yatajengwa kwa kulizunguka eneo litakalojengwa katikati litakaloezekwa. Hapa sehemu ya michezo iliyoezekwa itajengwa. Ujenzi wa uwanja wa mpira utakuwa mpango wa baadaye kidogo. Miti itapandwa kuzunguka eneo lililokamilika ujenzi kwa ajili ya kuleta sehemu za kutosha zenye vivuli . Kando ya nyumba za kuishi za watoto,na kando ya nyumba ya mikutano, ZAC inapanga kuongeza nyumba zingine, nyumba kwa ajili ya karakana ya ufundi, ( ufundi seremala na ushonaji) nyumba ya kuishi kwaajili ya Msimamizi mkuu wa kituo, na ofisi ya kiongozi wa kituo/kijiji. Nyumba ndogo ya mapokezi, gereji yenye vifaa vya kutosha na duka la vifaa mazao shamba karibu na mapokezi ya kituo. Duka la mazao shamba litakuwa kwa ajili ya kuuza mazao yatakayobaki yatakayozalishwa kituoni kwenye shamba la kituo pamoja na mifogo na matunda kwa watu wa eneo la Lutindi.

Kutakuwa na maeneo kwa ajili ya nyumba za wanyama wa kufugwa kwa ajili ya wanyama wadogo kama mbuzi na kuku,, bustani ndogondogo, kwanza haya yote yanapangwa kufanyika kwa ajili ya kuzalisha chakula kwa ajili ya kituo na sehemu itakayobaki itakayozalishwa kutoka kwenye kilimo na ufugaji, na bidhaa zitakazozalishwa kwenye karakana ya Useremala na ushonaji zitauzwa kwenye duka shamba la kituo.

Haiwezi kwenda bila kusema kwamba kituo kitahitaji miundombinu yake. Chumba kwa ajili ya nishati kitakuwepo cha teknolojia ya sola kusambaza umeme kwenye kituo. Nishati itakayozalishwa kutokana na sola haiwezi kutumika tuu kwa matumizi ya kijiji pekee, inaweza pia kuuzwa kwa wanakijiji kwa ajili ya kuchaji simu, kwa mfano kununua chakula kutoka kwenye vijiji kama sehemu ya kubadilishana.

Sehemu ya kuhifadhia maji itajengwa, itahusisha pia mashine za kuvuta maji (pampu) na teknolojia ya kuchuja maji inayoitwa (PAUL system) kusambaza maji safi na salama kwenye kituo. Maji yatatokana na chanzo safi cha maji tiririka yanayototiririka kandokando ya milima karibu na eneo la kituo cha watoto. Maji kwa ajili ya usafi yatapatikana kutokana na mvua. Kisima cha maji kitajengwa kwa ajili ya kuvuna maji ya mvua, maji haya pia ni kwa ajili ya matumizi ya umwagiliaji kipindi cha ukame kwenye eneo la bustani ya kituo.

Kwa baadaye, na kwa ajili ya kuhakikisha uimara endelevu wa kifedha wa shirika, majengo mawili ya ziada kwa ajili ya nyumba za kulala wageni yatajengwa kama hatua ya baadaye. Watalii watakodisha vyumba wale ambao watapenda kutembelea uzuri wa asili wa Tanzania na wanyamapori na pia itatumika kama shemu ya kuiwezesha taasisi kifedha. Nyumba hizi pia zinaweza kutumika kama nyumba kwa ajili ya wafanyakazi wa kujitolea wa shirika.