Kijiji cha Watoto Tanzania

Sisi, Zebras Active Community e.V. (kwa kifupi ZAC),shirika la kiserikali, (NGO)Tuna mpango thabiti kwamba, tutafadhili ,na kujenga kituo salama ambacho kitakuwa makazi kwa watoto hadi 60 mahususi wanaotoka kwenye mazingira magumu Tanzania.

Eneo la ujenzi lenye ukubwa wa ekari 20 lenye hati miliki namba 15172 ambalo limesajiliwa tayari kwa msajili wa Ardhi Tanzania tarehe 18.06.2020 kwa Shirika letu lisilo la kiserikali la Tanzania ( NGO) “C.B.R.O.”, lipo kwa ajili yetu kwa kusudi hili. Eneo hili lipo katika kijiji cha Lutindi, Wilaya ya Korogwe, Mkoa wa Tanga, Kaskazini mashariki mwa Tanzania. Eneo lipo kwenye mazingira bionuwai kwenye kingo za milima ya Usambara mashariki, urefu wa mita 1430 kutoka usawa wa bahari. Tumepewa eneo hili na kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited ( MeTL) moja ya waajiri wakubwa nchini Tanzania.

Tunataka kuhakikisha kwamba watoto ambao wengi wao ni yatima, katika kijiji/kituo chao, na kwa kuishi katika makundi madogo ya kifamilia wanaishi kwa kutunzwa kwa upendo, kupata lishe bora na kupatiwa mahitaji yote muhimu yanayohitajika ili motto aweze kukua katika afya bora na kuishi kwa furaha. Lakini sio hivyo tuu, kwa kuongezea, tungependa kuchukua sehemu ya jukumu muhimu kijamii kwa kutoa msaada katika kuboresha matarajio ya baadae ya watoto..

Kwa hiyo, ZAC inataka kusaidia sio tuu kufadhili sio elimu ya shule tuu ambayo kwa sehemu inalipiwa, lakini pia kuwasaidia vijana wanapaswa kuweza kutambua na kukuza nafasi mpya za maisha katika kijiji/kituo cha watoto chenyewe. Hii ni dhidi ya msingi kwamba wataalamu hususani wa ufundi nchini Tanzania wanahitajika kwa wingi na wana nafsi nzuri kuweza kufanikiwa kwa siku zijazo.

Kwa uthibitisho unaotambulika kiserikali, baada ya kumaliza elimu ya msingi, Karakana ya ufundi stadi yenye vifaa vyote vya kujifunzia itajengwa katika eneo la kijiji/kituo cha watoto (angalia picha kwenye “Mipango ya fedha”), ambapo watoto wanaweza kujifunza Ujuzi kwa vitendo katika tasnia ya uchomeleji vyuma. ZAC haitafadhili tuu katika kuajiri wakufunzi/walimu waliofuzu, lakini pia itatumia mafunzo na ofa ya chuo cha ufundi kinachoitwa HSBK-Oberhausen kilichopo Ujerumani katika kusaidia kikamilifu katika mafunzo ya juu zaidi katika ufundi stadi. Pia chumba cha mafunzo ya ushonaji wa nguo ambapo uzalishaji/ushonaji wa nguo katika kiwango cha kawaida,kimepangwa kujengwa.

Kwa kuongezea, watoto katika kijiji/kituo chao watakuwa na fursa ya kufanya kilimo na ufugaji wa wanyama wa kufugwa, kama sehemu ya kukuza stadi za kazi za mikono katika shamba darasa katika kijiji/kituo chao. Kama kila kitu kikienda kulingana na mpango, kijiji/kituo cha watoto kitakuwa na uwezo wa kupata mapato angalau kidogo kutokana na uzalishaji na uuzaji wa bidhaa ambazo zinazalishwa katika kijiji/kituo chake, kwa hiyo kwa sehemu flani hii itasaidia kituo kiuchumi.

Kanuni zinazoongoza ZACkatika shughuli zake zote ni kuwapa watoto uwezo wa kujitegemea wenyewe ,kuwa na amani, kuwa na hali nzuri kiuchumi,na kuishi katika mazingira salama. Hii ndio tunayomaanisha kwamba ni msaada endelevu wa kujisadia kwa mustakabali wenye hadhi/tija.